KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHMA MWENYE KUREHEMU
MIONGONI MWA MANENO YA HEKIMA YA MHESHIMIWA
SAYYID SWADIQ SHIRAZY (MUNGU AMZIDISHIE UMRI)

Hakika Mtume wa Uislaam (s.a.w) aliupatia ulimwengu Zawadi yenye thamani kubwa na ya aina ya pekee, na ndani ya Zawadi hiyo mna Saada na mafanikio kwa wanadamu wote, nayo ni Nidhamu, Hukumu na Kanuni mbali mbali alizo zithibitisha na kuwawekea Waislaam. Na kanuni hizo ni miongoni mwa kanuni na hukumu bora kabisa na zisizo na upungufu wa aina yoyote katika ulimwengu huu. Ili kuyajua hayo someni kwa jicho la udadisi mwenendo na historia yake (s.a.w) ili muweze kuona mamia kwa maelfu ya mifano mizuri ambayo lau kama itakusanywa yote kwa pamoja katika sehemu moja, mtu yeyote asie kuwa Muislaam hata kama atakuwa na asabia ya dini yake ataweza kuathirika na mifano hiyo na kuamua kujiunga na Uislaam (Kusilimu).
Kwa hivyo basi ikiwa itawezekana katika ulimwengu wa leo kufuatwa na kutekelezwa mfumo na wa Mtume mtukufu (s.a.w), na pia mfumo sira ya Amirul-muuminiin Ali bin Abi Twaalib (a.s) katika majumba yetu, sehemu zetu za kazi, katika mashirika, katika nchi zetu na miji yetu, kwa hakika yange thibitika yaliyo thibitika ulimwenguni kabla ya miaka 1400 iliyo pita, na hii ndio taawili (Tafsiri) ya kauli yake Mwenyezi Mungu alie takasika isemayo:

(ورأيت الناس يدخلون في دين الله أفواجا)

(Na utawaona watu wakiingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi)
Na mtaona ya kuwa watu maelfu kwa maelfu kama si mamilioni watakuwa wakiingia katika dini ya Uislaam.