UFAFANUZI WA KIONGOZI WA JUU WA KIDINI MHESHIMIWA AYATULLAHIL-UDHMAA SAYYID SWAADIQ AL-HUSEINIY SHIRAZIY MWENYEZI MUNGU AUREFUSHE UMRI WAKE KUTOKANA NA MNASABA WA MAOMBOLEZO YA ASHURA YA IMAMU HUSEINI (A.S) MWAKA 1427 HIJIRIA


 

الحمدلله رب العالمين وصلى الله على خير الخلق أجمعين محمّد المصطفى وعترته الطاهرين
ولعنة الله على أعدائهم أعداء الله الى يوم الدين

 

Imepokelewa katika hadithil-qudsi kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu-kuhusiana na ziara ya siku ya Ashuraa-:

اللهم اجعلني عند ك وجيهاً بالحسين عليه السلام في الد نيا والآخرة

(Ewe Mwenyezi Mungu nifanye mimi niwe mwenye hadhi na nafasi ya juu kwako kwa baraka za Huseini (a.s) duniani na Akhera). (Shekh Tuusiy (radhi za allah ziwe juu yake) katika kitabu Misbahul-mujtahidi ukurasa 774).
Ashura ya Imamu Huseini (a.s) ni utamaduni, thaqafa, na historia, na utamaduni huu umebeba na umekusanya mamabo makubwa yenye thamani.
Ama thaqafa ya Huseiniyyah imefichika kwenye malengo ya hali ya juu ya Imamu Huseini (a.s) yaliyopelekea kisimamo chake kitukufu kwani imepokelewa kwenye Ziyara ambayo Imamu Swaadiq aliamuru itumike katika kumzuru babu yake Imamu Huseini (a.s) nae akimzungumzia na kumhutubia Mwenyezi Mungu alie takasika na mtukufu: Na akajitolea muhanga nafsi yake katika njia yako ili aweze kuwaokoa waja wako kutoka kwenye ujinga na utata wa upotovu shaka upofu na shaka au wasiwasi na kuwafikisha kwenye mlango wa uongofu na kuwaepusha na upotovu). (Ibnu Qawlawaihi (radhi za allah ziwe juu yake) katika kitabu (Kaamiluz-ziyaarati) ukurasa 401- hadithi 639).
Kwa hivyo basi kuwaokoa waja wa Mwenyezi Mungu alie takasika, kutokana na aina zote za upotovu ujinga shaka upofu na wasiwasi ndio lengo la Imamu Huseini (a.s) la (kisimamo cha Ashura).
Na haya hayawezi kuthibiti isipokuwa kwa kuieneza na kuisambaza thaqafa na utamaduni huu kwenye ardhi yote mpaka watu wote waweze kupata saada kwa kuwa na imani sahihi na matendo mema na tabia iliyo bora jamii bora na ya kupigiwa mfano na idara au utawala wenye busara.
Na kwa hakika kumechomoza na kuenekana mashindano ya kutaka kulifanikisha hilo sana katika miaka khamsini ya mwisho kuliko hapo kabla katika nchi nyingi za ulimwengu na hiyo ni kutokana na baraka za majaalisi na vikao vya Imamu Huseini (a.s) na kudhihirisha shiari na alama zake, na hiyo ni kutokana na kutangazwa kwa thaqafa hii ya Mwenyezi Mungu-kwa hiyari na kwa kulazimika-katika mabara yote.
Na katika kila zama kumekuwa na habari zipokelewazo na kutufikia kwa wingi na zionekanazo kuhusiana na kufanywa na kusimamishwa majaalisi na vikao ya Imamu Huseini katika sehemu mbali mblai za ulimwengu hata kwenye maeneo yaliyo ganda ya barafu yaliyo kuwa karibu na miamba ya barafu ya kusini. sehemu ambazo daraja ya hali ya hewa ya baridi hushuka hadi kufikia daraja kumi chini ya sufuri.
Ndio: Lengo hili litathibiti kiukamilifu na katika kila sehemu pale atakapo dhihiri Sayyid na bwana wetu na maula wetu Baqiyyatullahil-aadham atokanae na kizazi kitwaharifu ambae ni Imamu Mahdiy (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake kutukufu) ili aweze kuijaza ardhi uadilifu na usawa, kwani usawa na uadilifu ni katika alama na shiari za babu yake Imamu Huseini (a.s).
Ama utamaduni wa Huseiniyyah: Unadhihiri kwa uwazi kabisa-pale unapo dhihiri- kupitia njia ya Mwenyezi Mungu kumpatia Imamu Huseini (a.s) kwa ajili ya Ashuraa nakutokana na kujitolea kwake muhanga kuliko kukubwa, na kumpatia baadhi ya sifa za aina ya pekee ambazo ndizo zilizo ujenga utamaduni huu mpana na wenye kuendelea katika nyanja nyingi, na hii ifuatayo ni baadhi ya mifanp hai:
Wa kwanza: Mwenyezi Mungu alie takasika na mtukufu amewafanya maimamu tisa maasumini (a.s) baada ya Iamamu Huseini watoke kwenye uti wa mgongo wake (watokane na kizazi chake: Kwa mfano Imamu Sajjad mwenye kitabu kiitwacho (Swahifatus-sajjadiyyah) Zaburi ya Aalu Muhammad (s.a.w.w) anatoka katika uti wa ngongo wa Imamu Huseini (a.s).
Na maimamu wawili Muhammad bin Ali Al-baaqir na Jaafar bin Muhammad As-swaadiq (a.s): waenezaji wa elimu ya mbinguni katika ardhi wao wawili wanatoka katika kizazi na uti wa mgongo wa Imamu Huseini (a.s).
Na Imamu Musa bin Jaafar Al-kaadhim (a.s): Ambae alidhihirisha na kubainisha uongo wa utawala wa bani Abbas walipo kuwa katika kilele cha utawala wao anatokana na kizazi na uti wa mgongo wa Imamu Huseini (a.s).
Na Imamu Ali bin Musa Ar-ridhaa (a.s): Mwanazuoni wa Aali Muhammad (s.a.w.w) kama alivyo sifiwa na babu yake Imamu Swaadiq (a.s) na ambae alifanya mahojiano na majibizano na mjadala na kuwashinda maulamaa wakubwa wa dini mbali mbali katika wakati mmoja na kuthibitisha ubatili wa itikadi zao na kwa kufanya kwake hivyo akaweza kuliinua neno la Uislaam-yeye pia anatokana na kizazi na uti wa mgongo wa Imamu Huseini (a.s).
Na Imamu Muhammad bin Ali Al-jawaad (a.s): ambae alipambana na tatizo la uasi katika umma na kulitokomeza na kuuokoa pia kuutoa umma kwenye tatizo hilo na kuufikisha umma kwenye imani safi, na kwa kufanya hivyo aliifasiri hadithi tukufu kutoka kwa baba yake Imamu Ridhaa (a.s) aliyo isema katika kuzaliwa kwake alipo sema: (Mtoto huyu alie zaliwa na ambae hakuna mtoto yeyote mwenye baraka kubwa juu ya mashia wetu kuliko yeye alie wahi kuzaliwa). Nae anatokana na kizazi cha Imamu Huseini (a.s).(Al-kafiy juzu 1\ 321 ).
Na Imamu Ali bin Muhammad Al-hadiy (a.s): ambae aliuokoa umma wa kislaam kutokana na Twaghuuti dhalimu alie ijaza miji kwa sharri, na kuwajaza waja kwa dhuluma na akawa mahiri katika kuanzisha aina tofauti za adhabu na matezo. Na ambae alitajwa na Imamu Amiril-muuminiin (a.s) katika hotuba yake na kumsifia kwa sifa ya (Mtu kafiri sana kati ya bani Abbasi) nei si mwingine bali ni Mutawakkili Al-abbas na kumuombea maangamizi na kusoma aya hii tukufu:

(تَمَتَّعُواْ فِي دَارِكُمْ ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ ذَلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ )

(Stareheni katika majumba yenu kwa muda wa siku tatu hiyo ni ahadi isiyo kosea na kwenda kombo) (Suurat-huud (a.s) aya 65). Na Mutawakkili kuuwawa baada ya siku tatu-imamu huyu anatokana na kizazi cha Imamu Huseini (a.s).
Na Imamu Hasan bin Ali Al-askariy (a.s): ambae aliwaokoa na kuwakomboa waislaam kutokana na hadaa za maulamaa wa kikiristo katika tukio la kuomba kunyeshelezewa mvua tukio lililo mashuhuri (Buharul-anwaar juzu 50\ 271). na kuwaokoa kutokana na mwanafalsafa alie maarufu (Al-kindiy) katika kitabu (Tanaaqudhil-qur’ani) (Buharul-anwaar juzu 50\ 311). kama ambavyo aliandaa mazingira kwa ajili ya mapokezi makubwa na kwa mapenzi makubwa: kuanzia pale Imamu Mahdi alipo kuwepo (a.s) hadi zama za kughibu kwake- nae huyu anatokana na kizazi cha Imamu Huseini (a.s).
Na Imamu Mahdi Al-hujjatu binil-hasan, alie ahidiwa na mwenye kusubiriwa ambae ndie Imamu wa zama hizi Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake- ambae kwa baraka zake viumbe wanapata riziki zao na kutokana na kuwepo kwake ardhi na mbingu vimethibiti- yeye anatokana na kizazi cha Imamu Huseini (a.s).
Mfano wa pili: Ardhi ikanyagwayo na miguu imefanywa kuwa takasifu kwa kuuliwa Huseini hadi Mwenyezi Mungu akakufanya kusujudu juu yake ni sababu ya kuinuli kwa sala na kukubaliwa na kufanywa kuwa ni dawa na shifaa ya kila gonjwa, kwa mfano imepokelewa kwenye hadithi tukufu:

(السجود على طين قبر الحسين عليه السلام يخرق الحجب السبعة)

(Kusujudu juu ya udongo wa kaburi la Huseini (a.s) huvuka na kuondoa vizuizi na hijabu saba) (Buharul-anwaar juzu 85\ 153 hadithi ya 14.) na imepokelewa katika haditthi nyingine:

(كل طين حرام.... إلا طين قبر الحسين عليه السلام فإن فيه شفاءاً من كل داء )

(Udongo wote ni haramu….isipokuwa udongo wa kaburi la Huseini (a.s) hakika ndani ya udongo huo kuna tiba na shifaa ya kila gonjwa) .(Al-kafiy juzu 6\ 378).
Mfano wa tatu: Hakika Mwenyezi Mungu alie takasika alimuhusisha tu Huseini (a.s)- kwa yale aliyo muhusisha nayo kutokana na kujitolea kwake katika njia ya Mwenyezi Mungu-na akalifanya kaburi lake kuwa ni mahala pa kujibiwa maombi na dua, kwa mfano imepokelewa katika hadithi tukufu ya kuwa Imamu Swaadiq (a.s) alipatwa na maumivu akawaamuru alio kuwa nao wamuajiri mtu ambae atamuombea Imamu kwenye kaburi la Imamu Huseini (a.s) (9).(Wasaailush-shia juzu 14\ 537).
Ama kuhusiana na historia ya Husein (a.s): Ni jambo lisilo shaka kuwa hakuna historia iliyo nzuri na kumeremeta mfano wa historia ya Imamu Huseini (a.s): Tangu Imamu Huseini alipo kufa shahid (a.s) hadi hivi leo-kiasi cha karne kumi na nne- kuna mamilioni… kwa mamilioni huongoka kwa sababu ya Imamu Huseini (a.s) na katika majlisi zake na kutokana na athari za shiari zake, na katika upande mwingine kuna mamilioni… kwa mammilioni ya watu wenye kumzuru Imamu Huseini (a.s) na wasimamishao shiari zake na wakaao kwenye majlisi zake-katika kipindi hiki kirefu-kilicho jawa na hali ngumu mateso adhabu za kila aina na dhuluma kutoka kwa mataghuti na watawala waovu walio jitokeza katika historia, kwa kuanzia na mataghuti wa bani umayyah hadi kufikia mataghuti wa bani Abbas hadi hivi leo katika sehemu mbali mbali za ulimwengu, kwa hakika historia katika uwanja huu imekusanya mambo mengi sana mambo ambayo huufanya uso wa mwanadamu kuhuzunika, na kati ya mambo yaliyo tajwa ni kuwa Mutawakkili Al-abbasiy aliamuru kupigwa kwa (Nasru bin Ali) fimbo elfu moja kutokana na kupokea na kusimulia kwake hadithi moja kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na fadhila za Imamu Huseini (a.s),(Al-kunaa wal-alqaab juzu 1 \ 415). pamoja na yote hayo tunaishuhudia ardhi-katika mabara yote-ikinyekenya kwa majaalisi na vikao na shiari za Imamu Huseini (a.s) kwa miaka yote hiyo na hasa katika siku za Ashuraa).
Kwa hivyo basi ni juu ya watu wote kila mahala-kila mmoja kwa kiwango chake na kutokana na nafasi aliyo nayo na kutokana na uwezo wake-kutilia hima kubwa suala la kuhifadhi na kulinda thaqafa na utamaduni huu na calture hii na historia hii huenda kwa kufanya hivyo watu hao wakajibiwa dua iliyo tajwa katika zaiara ya Ashuraa, na kuwa-sisi sote kuwa ni watu wenye nafasi za juu kabisa na hadhi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu katika dunia na akhera kwa baraka za Imamu Huseini (a.s).
Na Mwenyezi Mungu ndie aombwae kuwapatie wote tawfiiq ya kuweza kusimamia majukumu haya matukufu kwa namna inayo takiwa kutokana na hadhi pia cheo cha Muhammad na Aali zake Muhammad na hasa walii wa damu ya Imamu Huseini (a.s) bwana wetu na maulana wetu swaahibul-amri imamu wa zama Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake na faraja yake tukufu.


SWAADIQ Al-SHIRAZIY
1\ muharramul-haraam / 1427 hijiria.