SALAM ZA RAMBIRAMBI ZA MARJIU WA JUU WA KIDINI MHESHIMIWA SAYYIDI SWAADIQ SHIRAZIY KUTOKANA NA KITENDO CHA UCHOKOZI KILICHOFANYIKA KWENYE MAKABURI YA MAIMAMU WAWILI Al-HAADI NA ASKARI (A.S).

Kutokana na uchokozi wa kidhalimu na wakiwoga ulio fanywa kwenye makaburi matukufu ya Imamu Al-hadi na Al-askariy (a.s) na ambao ulifanywa na kikundi cha sharri na madhalimu na kikufurishacho waislaam (At-takfiiriyyah), na maadui wa ahlul-baiti (a.s), asubuhi ya siku ya juma tano iliyo sawa na tarehe 23 ya mwezi wa Muharram mwaka 1427 hijiria, Marjiu na kiongozi wa juu wa kidini mheshimiwa Ayatullahil-udhmaa sayyid Swaadiq Al-huseiniy Al-shiraziy (Mungu amzidishie umri) alitoa salam za rambarambi na kemeo la kupinga tukio hili ovu, akimtaraji Mwenyezi Mungu mtukufu aweke mbadala kati ya waislaam watu watakao weza kusimama kidete dhidi ya vitendo kama hivi kwa mjia mbalimbali za kisheria na kutokana na jukumu na wadhifa wa kiislaam.na ifuatayo ni barua na kemeo lenyewe:

 

بسم الله الرحمن الرحيم

 

إنالله وإنا إليه راجعون

 

{ وسيعلم الذين ظلموا أي منقلب ينقلبون والعاقبة للمتقين}

Katika Mwezi mtukufu wa Muharram ambamo ndani yake imevunjwa heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwani ndani ya mwezi huu ndimo ilipo halalishwa kumwagwa damu ya mjukuu wake Imamu Huseiniy (a.s), ndani ya mwezi huu madhalimu wamesimama na kuyabomoa kwa mabomu makaburi matwaharifu ya maimamu wa waislaam ambao ni Imamu Ali bin Muhammad Al-hadiy na Imamu Hasan bin Ali Al-askariy (juu yao rehma na amani) katika mji wa Samarraa katika siku hii. Kama ambavyo Mutawakkili Al-abbasiy alivyo bomoa kaburi tukufu la Imamu Huseiniy (a.s) huko Karbalaa tukufu  na kuvunja kisha kubomoa makaburi ya maimamu watwaharifu (juu yao rehma na amani) katika Baqii’i.

 

Kwa hakika kutokana na tukio hilo natoa salam za rambi rambi na pole kwa Bwana wangu na mtawala wangu walii wa Mwenyezi Mungu atakae lipiza kisasi hoja wa Mwenyezi Mungu alie bakia atokae katika kizazi kitukufu Mwenyezi Mungu aharakishe faraja na kudhihiri kwake kutukufu na ninatoa salama za pole kwa majonzi na huzuni kubwa na maumivu makubwa kutokana na msiba huu mkubwa na uovu huu mbaya kutokana na matendo haya yasiyo kuwa ya kibinadamu na yasiyo jali utu.

 

Na namtaraji Mwenyezi Mungu mtukufu atoe mbadala katika waislaam watu watakao simama kidete na kuzuia mfano wa matendo kama haya kwa njia za aina tofauti za kisheria na kwa mujibu wa wadhifa wa kiislaam katika uwanja huu na hakuna mwenye nguvu wala uwezo na nguvu isipokuwa Mwenyezi Mungu mtukufu na wa juu.

 

SWAADIQ Al-shiraziy.

Juma tano tarehe 23\ Muharram\ mwaka 1427 hijiria.