OFISI YA MARJIU NA KIONGOZI WA JUU WA KIDINI MHESHIMIWA SAYYID SWAADIQ SHIRAZIY INAKEMEA NA KULAANI VIKALI TENDO OVU LILILO FANYIKA KWANYE MAKABURI YA IMAMU AL-HADIY NA AL-ASKARIY NA INAWAOMBA WATU WOTE KUOMBOLEZA KUTOKANA NA TUKIO HILI NA INAZIOMBA SEHEMU HUSIKA NA WASIMAMIZI KUSIMAMA KIDETE DHIDI YA MATERORISIM

Kutokana na uovu uchukizao ambao ulifanywa na maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui wa Mtume wake mtukufu na Ahlil-baiti wake watwaharifu (rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao) katika uadui na uchokozi wao wa kidhalimu walio ufanya kwenye makaburi matwaharifu ya maimamu wawili Imamu Al-hadiy na Al-askariy (a.s) katika mji wa Samarraa asubuhi ya tarehe 23 ya mwezi wa Muharram mwaka 1427 hijiria, ofisi ya Marjiu wa juu wa kidini mheshimiwa Ayatullahil-udhmaa Sayyid Swaadiq Al-shiraziy (Mungu amzidishie umri) iliyoko katika mji mtukufu wa Qum inatoa kemeo la kulaani uovu huu na kuwaomba watu wote kuzindukana na kufuata maelekezo ya Maraajiu na viongozi wa juu wa kidini na kuomboleza wote kwa ujumla, na kuziomba sehemu husika kusimama kidete dhidi ya materorisim na kuto salenda kwa ajili yao, na ifuatayo ni barua ya kemeo la kulaani kama ifuatavyo:
Hakika tukio ovu na baya la kubomolewa kwa mabomu haramu mbili za Imamu Ali Al-hadiy na Imamu Hasan Al-askariy (a.s), na kuiharibu Kuba yenye nuru na Dharihi tukufu, hakika si vinginevyo bali huko ni kuendelea kwa majaribio ya Manawaasiib (Maadui wa Ahlul-baiti ) la kuvunja heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), ukianzia na kuvunjwa heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa kumuulia kizazi chake katika ardhi tukufu ya karbalaa, na kumalizia kwa kuharibu na kubomoa makaburi yao kama alivyo fanya Al-mutawakkili Al-abbasiy kwa kuvunja kaburi la Imamu Husein (a.s), na kama walivyo fanya Mawahabi kwa kuharibu kubomoa na kuvunja makaburi ya maimamu wa waislaam kama vile Imamu Hasan Al-mujtaba na Imamu Sajjad Zainul-aabidiin na Imamu Baqir na Imamu Swaadiq (a.s) katika makaburi ya Baqii’i?
Na sisi tunakemea na kulaani tendo hili ovu na tunawakumbusha waumini watukufu yafuatayo:
1-Hakika tawala zenye nguvu na za sharri huenda zikajaribu kufaidika na maovu haya kwa ajili ya kuhamasisha mapigano ya kikabila na kuwasha moto wa vita vya ndani ya nchi na huo ukiwa ni utangulizi wa kuigawa iraq, kwa hivyo basi ni juu ya wote kuamka na kuwa macho na kujihadhari na kufuata maelekezo ya Maraajiu na viongozi wa juu wa kidini na kufanya kazi kufuatana na kanuni na vidhibiti vya kisheria na kuto fanya vitendo viovu dhidi ya misikiti ya madhehbu na makundi mengine.
2-Kuyaomba Madola mbalimbali ya kiislaam na mengineyo kukemea na kupigana na kupambana na uterorisim na kusimama kidete dhidi ya uterorisim na kuangamiza mizizi yake na kutoutumia kama nyenzo na wasila wa kufikia kwenye malengo ya kisiasa.
3-Watu wote kuomboleza na kufunga maduka na kutoka kwa kufanya maandamano ya amani na kuzitumia barua na fax taasisi mbalimbali za kidini za kiislaam na taasisi zinginezo na taasisi za kimataifa ili zikemee na kulani uovu huu mkubwa.

4-Kuzitaka na kuziomba sehemu husika kusimama kidete dhidi ya materorisim na kuto salenda na kuwapa nafasi mpaka materorisim wafahamu ya kuwa uterorisim wao hautakuwa ni sababu ya kuwapatia nafasi ya kisiasa kama malipo ya matendo yao na ili weweze kuachana na matendo kama haya maovu.
5-Kuharakisha kuijenga na kuikarabati Haramu tukufu, na kwa namna iliyo bora zaidi iwezekanavyo, na kuwashitaki wahusika ambao walizembea katika kulinda usalama wa mahala hapo, na kutekeleza sheria na kanuni za mahala patakasifu (Atabaatil-muqaddasah).
Na mwisho tunatoa tena salam zetu za pole kwa Imamu Al-hujja mwenye kungojewa (Mwenyezi Mungu mtukufu aharakishe kudhihiri na faraji yake tukufu), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu alipizie kisasi kwa watu hawa waovu kama alivyo ahidi alie takasika:

 

 (إنا من المجرمين منتقمون»

 

(Hakika sisi ni wenye kulipiza kisasi kwa watu waovu) na aviangamize vitimbi vya maadui na kuvirudisha kwenye vifua vyao, na aiokoe nchi ya Iraq na kuielekeza kwenye Imani uhuru maisha bora na amani.
Offis ya mheshimiwa Ayatullahil-udhmaa
Swaadiq Al-huseiniy Al-shiraziy mungu aurefushe umri wake.
Qumil-muqaddasah.
Tarehe 23 \ Muharram \ mwaka 1427 hijiria