KIKUNDI CHA WANAFUNZI WA KIAFRIKA WALIPO KUTANA NA MHESHIMIWA

AYATULLAHIL-UDHMAA SAYYID SWAADIQ SHIRAZI

JUHUDI ZA KUWAONGOA WATU NI BORA ZAIDI KULIKO KUTOSHEKA NA IBADA PEKEE.

 

 

Kikundi cha wanafunzi wa  kidini wa kiume na kike wa kiafrika waishio katika mji mtukufu wa Qum walimtembelea mheshimiwa kiongozi wa juu wa kidini ayatullahil-udhmaa sayyid Swaadiq Al-huseiniy Shirazi (Mwenyezi Mungu amzidishie umri). Na baada ya mheshimiwa  kuwakaribisha alianza  na kufungua mazungumzo yake kwa kusoma aya tukufu isemayo:

(Na siku ambayo litafufuliwa kundi kutoka kila ummati)

kisha akasema: imeelezwa na kupokelewa katika taawili na tafsiri ya aya hii tukufu ya kuwa pindi atakapo dhihiri sayyidi wetu na maulana  Imamuz- zamani Al-muntadhari (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), na ninamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu nasi tukiwa kwenye kumbukumbu za kuzaliwa kwake atujaalie tuwe katika wasaidizi wake na jeshi lake na atujaalie kupata ridhaa yake na uangalizi wake. 

Na baada ya Mheshimiwa kutaja riwaya kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) alibainisha ubora wa muumini mwenye elimu mwenye kujishughulisha tu na ibada kisha akasema:

Kabla ya ya miaka takriban 150 iliyo pita alizaliwa mtu mmoja katika familia ya kikiristo na kukua katika familia hiyo na akasoma elimu za kikiristo na kufikia kuwa padri na kupata nafasi ya juu kabisa  na kuwa raisi wa kanisa  na alipata kuwa na mahusiano na mawasiliano na mwanazuoni mmoja wa kishia na baada ya kufanya nae majadiliano na mazungumzo ya muda mrefu na kwa mara kadhaa yule mkiristo aliongoka na kufuata madhehebu ya kishia  na kubadili jina lake na kuitwa Muhammad Swaadiq na kutunga kitabu alicho kiita kwa jina la (Aniisul-aalam fii nusratil-islaam) katika kitabu hicho alibatilisha  ndani yake dini ya ukiristo na kubainisha kisha kufafanua ukweli wa uislaam, na kwa sababu ya kitabu chake hicho wakiristo wengi waliweza kuongoka na kujiunga na dini ya kliislaam. 

Na mheshimiwa aliendelea na kusema: Hakika aliyo yafanya mwanazuoni huyu wa kishia katika kumuongoza mkiristo huyo na kuingia kwenye madhehbu ya kishia ni bora zaidi kuliko kama ange kaa tu na kutosheka na kufanya ibada pekee. 

Kisha Mheshimiwa akataja kisa cha kusilimu kwa sahaba mtukufu na mkubwa Abi Dharril-ghaffariy radhi za Allah ziwe juu yake na mambo aliyo pambana nayo kama dhuluma na unyanyasaji kwa sababu ya kushikamana kwake na wilaya ya Amiril-muuminiina (a.s) na kwamba yeye aliweza pekee kupandikiza mbegu za ushia katika nchi ya Lebanoni pamoja na matatizo ya ugeni na kuhamishwa  na matatizo ya kufukuzwa hasa katika mazingira ya zama zile. 

Na mheshimiwa akasema : Hakika kutafuta elimu na kufanya tabligh au kueneza dini na kuwaongoza watu na kuwaelekeza kwenye hidaya hapo zamani ilikuwa ni kazi  na jambo gumu sana kutokana na sababu ya umbali na mazingara ya kiusalama na amani ambayo haikuwa ni nzuri na kutokana na uchache wa nyenzo, na hasa katika bara la Afrika ambalo ni pana na kubwa kwa mfano. Ama hivi leo jambo hilo limekuwa ni jepesi na rahisi kwa kiwango fulani, na hili ndio linalo fanya majukumu yaliyoko mabegani na katika mashingo yetu kuwa makubwa zaidi na zaidi.

 Na mheshimiwa akasisitiza kwa kusema: Kwa hivyo basi ni vema kwenu kufanya kila juhudi na kujitahidi kujifunza misingi ya Uislaam na hukumu zake na kanuni au adabu zake na madhumuni pia mafhumu yake ya hali ya juu kisha mfanye juhudi na sa’aai kwa ajili ya kuwaongoa watu wengine kwa kadri ya uwezo wenu na kwa kadri ya nyenzo mlizo nazo na mlizo pewa, na katika kufanya hivyo mfuate kigezo cha Abi dharri na masahaba wema wa maimamu wema juu yao rehma na amani. Na jambo hilo linahitaji kuwa na ikhlasi na usafi wa nia na uchapakazi na kupambika kwa tabia bora na njema na kujitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu alie takasika na mtume wake mtukufu na Ahli baiti wake watwaharifu juu yao wote rehma na amani.