HISTORIA FUPI YA MAISHA YA  MHESHIMIWA SAYYID SWAADIQ SHIRAZY

Yeye ni mwanazuoni  mwema na mtukufu na mlezi wa wanazuoni, na ni kiongozi wa kiroho Ayatullahil-udhmaa Sayyid Swadiq Mahdi Al-huseiniy Shiraziy, anaetokana na Nasaba (familia) tukufu kabisa katika ardhi hii: Nayo ni Nyumba na familia ya Mtume wa mwisho na Ali zake walio watwaharifu (a.s) rehma na amani ziwe juu yao. Kwani Nasaba yake inarejea kwa Imam Ali bin Hussein Zainul-abidiin rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.

Yeye ni mtoto atokanae na nyumba ya viongozi wa juu wa kidini (Usratul-marjiayyah) yaani familia ya maraajiu wakubwa  katika historia ya madhehebu ya Shia Imamiyyah, kwani familia hiyo ilichukua uongozi wa kidini tangu karne mbili zilizo pita ukianzia na Al-mujaddidil-kabiir wa kwanza Ayatullahil-udhmaa Sayyid Muhammad Hassan Shiraziy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Alizaliwa mwaka 1360 hijiria katika mji mtukufu wa Karbalaa mji wa babu yake Hussein (a.s) katika nyumba ya wacha Mungu, wana ijtihadi na wanazuoni wakubwa wa Fiqhi.

Nyumba ya Marjiu na kiongozi wa juu kabisa wa kidini Mheshimiwa Ayatullahil-udhmaa Sayyid Mirza Mahdi Shiraziy (Mwenyezi Mungu autakase utajo wake) ambae alimlisha na kumjaza elimu yake ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo yeye ndie alie kuwa mwalimu wake na mlezi wake wa mwanzo.

Tangu utotoni mwake alijishughulisha na utafutaji wa elimu ya dini akiwa na ufahamu wa hali ya juu kabisa ulio watia mshangao walimu wake wakubwa, nao wakiwa ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa: kama vile Sayyid Muhammad Hadiy Al-milaniy, na Shekh Muhammad Ridhaa Al-isfahaniy, Shekh Jaafar Rashiy, na Shekh Muhammad Shahrudiy (Mwenyezi Mungu autukuze utajo wake) na wengineo, wakati ambapo alikuwa ni mwanafunzi wa Marjiu wa juu kabisa wa kidini na alie kuwa mjuzi zaidi kati ya wanazuoni wa zama zake na mkubwa Ayatullahil-udhmaa Sayyid Muhammad Husseiny Shiraziy (Mwenyezi Mungu aiinue daraja yake), kwani marhum Sayyid alimpa hima ya aina yake na usaidizi wa pekee, na alikuwa ndie msiri wake na mtu pekee alie kuwa akimtegemea na aliekuwa na matumaini nae na akimuamini, kwani alifikia hatua ya kuwarejesha wafuasi wake katika ihtiyaati zake kwa Swaadiq katika zama za uhai wake, na akimzingatia kuwa tiyari kisha fikia nafasi ya juu kabisa katika ijtihadi na ujuzi wa elimu ya Fiqhi, na akawa mashuhuri kwa maneno yake yanayo sisitiza ya kuwa Swadiq ndie mjuzi kabisa baada yake.

Alifahamika katika Hawzatul-ilmiyyah kuwa ni mtu mwenye kipaji cha juu kabisa cha akili na mwenye ufahamu wa pekee na uliopita kiasi katika elimu ya Fiqhi na Usuul, na akawa mashuhuri katika Hawza hiyo kutokana na ubobeaji  wake wa kielimu na wa kina, hadi bahthi zake na masomo yake ya Khariji zikawa ndio zenye mustawa wa juu kabisa kati ya masomo ya hawza.

Na masomo pia bahthi zake zikawa ndio mahala wapishaniapo mamujtahidi na wanazuoni wengi tangu miaka zaidi ya ishirini na zaidi iliyo pita, na Mheshimiwa Sayyid bado anaendelea na utoaji wa darsa zake katika Hawzah ya kielimu katika mji mtukufu wa Qum, na kuna kundi kubwa kabisa la wanazuoni watukufu na wakubwa walio hitimu katika mikono yake, na ambao walifikia katika nafasi ya ijtihadi kwa umakini na umahiri na ufahamu mkubwa na wa hali ya juu.

Uchamungu wake na kujiepusha kwake na maasi na ladha za maisha ya kidunia na kumtakasia nia Mwenyezi Mungu (yaani kuwa na Ikhlas) na Mola mtukufu na kuwatawalisha kwake Ahlul-bayti watwaharifu kusiko na mipaka na wa aina ya pekee, yote hayo ndio yaliyowafanya maulamaa wakubwa wamtukuze na kumheshimu kwa kiwango kikubwa na kumhesabu kuwa ni katika mawalii wema wa Mwenyezi Mungu.

Vitabu vyake vya Fiqhi na Usuul alivyo viandika viliwafanya maulamaa wakubwa wa Hawzah washikwe na mshangao na kuwafanya wamsimamie kwa heshima na taadhima ya aina yake kati ya wanazuoni mfano wake, kutokana na umakini, undani  uzuri na ulio zihusu nyanja zote, na hasa sharhi yake kubwa ambayo ni Sharhul-ur’watul-wuthqaa ambayo ina mujallad kadhaa, pia kitabu chake kingine kilicho makini kijulikanacho kwa jina la Bayaanul-usuulil-waaqiu  chenye mijallad kumi, pia sherhe yake ya kitabu (Allum’ah) na (At-tabswirah) na ( Sharaaiu) na (Suyuutwi) na As-swamadiyyah) na (Al-mantwiq) na vinginevyo.

Baada ya kufariki kwa kaka yake mkubwa Ayatullahil-udhmaa Sayyid Muhammad Shiraziy (Radhi za Allah ziwe juu yake) waumini katika pande zote za dunia walimuelekea na kurejea kwake katika masuala ya dini, tangu wakati huo ushahidi wa maulamaa wakubwa wakubwa umekuwa ukifuatana na ushahidi wa wataalamu katika nyanja hizo ukithibitisha kuwa ni mtu alie Aalam (mjuzi zaidi) na kwamba anayo maandalizi ya kushika nafasi ya marjiu.

Na kitabu chake hiki (Haqaaiq ani Shia) ni kitabu ambacho amehoji na kuchambua ndani yake baadhi ya mas’ala yahusianayo na Ushia na tashayyui, na mheshimiwa Sayyid katika kitabu hiki ametumia mfumo wa mahojiano na mazungumzo kati ya watu wawili, mfumo wenye kuvutia na kwa sura ya muhtasari akiwa ametilia mkazo na kusisitizia katika nukta muhimu na mwepesi, kwa lengo la kuwaelekea na kuwahutubia au kuwazungumzia watu wote bila kubagua katika upeo wao wa maarifa na ili wote waweze kufaidika na kunufaika nacho, akitetea itikadi ya kweli na kwa kuzama kiundani katika kuyafahamu mafunzo ya dini.