UTANGULIZI

Ukoloni bado unaendela na kazi yake ya kutaka kutia fitina na kuupiganisha au kuugombanisha umma wa kiislaam, na bado unaendelea na uadui wake dhidi ya umma wa kiislaam kwa kuelekeza mambo yaliyo jawa na asabia kwa ajili ya batili na kuufarakanisha na kuutenganisha ili utawala wao mbaya ubakie katika nchi za kiislaam na ukitekeleza siasa ya kikafiri na isiyoridhiwa isemayo (Watenganishe ili uwatawale)!.

Kwa mfano utawaona baadhi ya Waislaam, na wao wakiwa ni ndugu kwa ushahidi wa Qur’ani tukufu, bila ya kufikiria na wakiwa na hamasa kubwa wakielekeza tuhuma za uwongo dhidi ya kikundi kingine cha Waislaam, kwa sababu kikundi kile au Madhehebu yale wanafuata Madhehebu mengine tofauti na madhehebu  yao, na wakifuata na kuchukua hukumu za Fiqhi kutoka kwa Imam mwingine tofauti na Imam wao, bila ya kufikiri wala kufanya utafiti juu ya ukweli wa uzushi huo, na bila kutumia muongozo wa nuru ya akili na sunna ya Mtume (s.a.w) iliyo sahihi.

Pamoja na kuwa ni wajibu kwa Waislaam katika zama zetu hizi- na ikiwalazimu na kuwawajibikia wao kuziimarisha safu zao na umoja wao, na kuungana pia kushikamana na kuyafanya malengo yao kuwa ni mamoja kwa ajili ya kumpiga vita mkoloni, na kuwafukuzia mbali wenye tama kati ya Waislaam, na wenye kuzitilia tama nchi za Waislaam.

Kama kuziimarisha safu zao za jeshi moja lenye kufuata serikali moja lililo undwa kwa madhehebu tofauti wakati linapo shambuliwa na adui wao wote kwa pamoja.

Ama masuala mengine mbalimbali katika serikali hiyo, na hukumu zingine ambazo wanatofautiana katika hukumu hizo kati ya makundi mbalimbali ya kiislaam, njia ya kutatua tofauti hizo ni mazungumzo na majadiliano yaliyo safi na yaliyo epukana na matusi na tuhuma, mazungumzo na majadiliano yaliyo simama juu ya misingi ya kiislaam na yenye kukubalika kwa Waislaam wote.  

Ama baadhi ya Waislaam kuwatusi na kuwatukana Waislaam wengine kwa sababu tu ya baadhi ya mas’ala ya tofauti ya kimadhehebu, au baadhi kuwakufurisha wengine kwa ajili ya hukumu isiyo ya ijmaai (isiyo kubalika kwa maulaa wote wa kiislaam), jambo kama hilo ndilo ambalo hupelekea kufarakana kati ya Waislaam na kuvunja umoja wao na kuvunja umoja wa kiislaam, umoja ambao ni jambo kubwa na adhimu.

Na katika kitabu hiki tutaonyesha baadhi ya nukta mbalimbali ambazo wamekuwa wakishambuliwa nazo Mashia Imamiyyah na baadhi ya watu wenye nia ya kuwatenganisha Waislaam, ili tuweze kuona kutokana na bahthi hii ubatilifu wake, na Mwenyezi Mungu ndie mwenye kutegemewa na kuombwa usaidizi katika njia yetu hii ili tuweze kuyaangalia mambo hayo kwa mtazamo wa kiislaam na atuwafikishe kuufuata, hakika yeye ni mwenye kusikia na mwenye kuitikia maombi.

 

          28\ Dhil haji\ 1380 hijiria

                     Karbalaa 

              SWADIQ SHIRAZIY