KUENEZA ITIKADI YA USHIA NI FURSA YA THAMANI SANA KATIKA UMRI WA MTU

 

YAPANGENI VEMA MAMBO YENU NA WALA MSIYAACHE HORERA [1]

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu.

Sifa zote njema zinamstahiki Mola wa viumbe wote na sala na salam ziwe juu ya bwana wetu Muhammad na Aali zake walio watwaharifu, na laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya maadui zao wote hadi kitakapo simama kiama.

ما عندكم ينفد وما عند الله  باق

(Mlivyonavyo vitakwisha na vilivyoko kwa Mwenyeezi Mungu ndivyo vitakavyo bakia) [2]

Aya hii ni miongoni mwa aya nyingi za kitabu kitukufu cha Allah na maana yake ni kuwa kila mlicho nacho ni chenye kutoweka na kumalizika bila shaka yoyote, na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni yenye kubakia milele. Kwa hakika katika usiku huu mmetekeleza na kusali sala mbili Maghribi na Isha, na Shekh Tusy (Radhi za Allah ziwe juu yake) alifariki na kuiaga dunia kabla ya zaidi y miaka elfu moja iliyo pita, lakini sehemu fulani ya thawabu za sala ya Magharibi na Isha mlizo zisali na kuzitekeleza ataandikiwa yeye, kwa sababu yeye alikuwa ni sababu ya kusaliwa sala hizi, kwani mas’ala mengi, pia Hadithi nyingi zilizo tufikia sisi zimetufikia kupitia kwake na kutokana na juhudi zake,

والدال علي الخير كفاعله

Na mwenye kuwaongoza watu kwenye kheri ni kama mfanyaji wa kheri hiyo (katika thawabu)

Ni watu wangapi walio fanikiwa kusali katika usiku huu wa leo?! Bila shaka yoyote ni mamilioni kadhaa, sasa angalieni kiasi cha thawabu ambazo atazipata Shekh Swaduq kutokana na sala hizi pekee. Si vibaya kueleza kuwa Marhum Shekh Tusy alikuwa na ndugu ambae alifahamika kwa wema wake na kwamba alikuwa ni mtu alie shikamana na dini vema, lakini ndugu yake huyo hakutuachia athari yoyote, (kumbukumbu yoyote) na wote wawili walikuwa ni watoto wa baba mmoja na wakiishi wakati mmoja, lakini mamilioni haya ya thawabu yanamfikia Shekh Tusy kila siku wakati ambapo ndugu yake hapati thawabu hizo, kwa sababu hakuacha athari wala chembe yeyote katika dunia kama alizo ziacha ndugu yake wa tumbo moja.

Na jaribuni kuangalia (fanyeni Taswawwur) ya kuwa baada ya miaka elfu moja tokea sasa ni nani utajo wake utabakia na nani atasahaulika na kuto kumbukwa kabisa, kwa hivyo basi nyinyi mnaweza hivi sasa kufanya mambo au matendo ambayo  yatakuwa ndio sababu ya kubakia  utajo wenu na mkawa ni wenye kukumbukwa kwa muda wa maelfu kadhaa ya miaka na mkajipatia thawabu zisizo koma na kumalizika na zenye kuendelea milele na bila kukatika.

Kwa hakika Mwenyezi Mungu alikadiria kuwa nchi ya India ibadilike na yote kugeuka  na kuwa nchi ya Kiislaam, (yaani watu wake wote wabadilike na kuwa Waislaam), katika siku za usoni, na vizazi vyote vijavyo visilimu, vizazi vitokanavyo na waabudu masanamu, kama vile wenye kuabudu Ng’ombe,  panya na wenye kuabudu jua.

Kwa mfano kabla ya miaka mia moja iliyopita nchi ya Iran yote ilikuwa ni nchi ya kikafiri na baada ya miaka mia moja ili badilika yote na wakazi wake wote wakawa ni Waislaam wa madhehebu ya sunni, kisha wananchi wake wakaongoka na wengi wao au asilimia kubwa kati yao hivi leo wakawa ni wafuasi wa Madhehebu ya Ahlul-bayti (a.s), na haya ndio yatakayo tokea katika nchi ya India vilevile, kwa utashi wake Allah.

Na hapa linajitokeza swali moja nalo ni kuwa: Baada ya miaka kadhaa, ni ipi nafasi yenu na dauru lenu katika mabadiliko hayo yatakayo tokea?!

Inasemekana kuwa katika nchi ya India kuna zaidi ya watu milioni 600 wenye kuabudu masanamu, sasa ikiwa mmoja wenu atachukua jukumu la kusoma vizuri kitabu kitukufu cha watu wenye kuabudu masanamu kisha baada ya kufanya hivyo akachukua jukumu la kukusanya vijana na mabarobaro ambao ni watoto wa wenye kuabudu masanamu katika nchi ya India na akawafafanulia yaliyomo kwenye kitabu chao kitukufu na akawatolea mihadhara, pia akawakusanya wanafunzi wa vyuo vikuu na walimu, pia wasomi, wabunge, mawaziri na watawala kwa kutumia mantiki ya akili na akasema: Je nyinyi mmekinaika na mafundisho haya yaliyomo kwenye kitabu chenu kitakasifu?! Na je mnafahamu ya kuwa mambo haya ya kutunga ni sehemu moja wapo ya itikadi yenu ya dini?! Niswadikisheni ya kuwa mmoja wenu anaweza kwa kufanya hivi kuziyumbisha Imani za maelfu miongoni mwao.

Nitakutajieni baadhi ya mifano hai kati ya mambo yaliyomo kwenye kitabu chao kitakatifu, na kati ya hayo ni kuwa:Ikiwa mwanamume ataoa mwanamke na baada ya muda mrefu mwanamke yule asifanikiwe kuzaa au asimzalie mtoto na baada ya kuonana na madaktari na kumsisitizia au kumthibitishia ya kuwa mwanamume hana kizazi yaani ni tasa, inajuzu kwa mwanamke yule kulala na ndugu wa kiume wa mumewe ili aweze kupata mtoto mmoja tu na si zaidi, na mtoto yule hunasibishwa na kuambatanishwa na mumewe! Na jambo hili ni lenye kupingwa na nafsi ya kila kiumbe na ghera (wivu) inapinga kitu kama hicho, pia elimu inapinga kitu kama hicho.

Na katika mahala pengine kitabu hicho kitakatifu kina sema: Wakati mwingine hutokea mwanadamu kubadilika na kuwa Mungu kiasi kwamba yeye mwenyewe hahisii hivyo au bila ya yeye kuhisia! Na jambo hili ni jambo la batili na lisilo na maana yoyote kwa kiwango kikubwa.

Hakika kitabu chao hiki kimejawa na mambo ya kutunga na ya batili na ngano zisizo na maana, na anaweza mmoja wenu kuyafuatilia kwa karibu zaidi na kujua idadi yake na kuyaeleza wazi wazi bila kutumia matusi na kejeli. Kwa hivyo basi mas’ala muhimu kabisa katika dunia ni kuwaongoza viumbe, na Mtume (s.a.w) alimwambia Imam Amiril-muuminiin (a.s): Ewe Ali ikiwa Mwenyezi Mungu alie takasika atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako ni bora kwako (ni kheri kwako) kuliko vitu vyote vichomozewavyo na jua (vipatavyo mwanga wa jua).[3]

Na ninakunukulieni kisa kingine, Imepokelewa katika moja wapo kati ya kitabu cha historia nacho ni (Atharul-bilaad wa Akhbaarul-ibaad) ya kuwa mtawala mmoja wa kisunni aliekuwa akitawala Iran  alitengeneza muhuri wa chuma na akachonga kwenye muhuri huo Ibara hii (Abubakar wa Omar) na alikuwa akiwaonea na kuwadhulumu Mashia na akiwatawala kwa mabavu pia alikuwa akiwapiga muhuri huo kwenye mapaji ya nyuso zao baada ya kuuchemsha kwa moto, na kitabu hicho kinasimulia ya kuwa baadhi ya Mashia ambao walipigwa mhuri huo kwenye mapaji ya nyuso zao walikuwa hawatoki majumbani mwao kwa muda wote wa maisha yao na hawakutoka wala kuyahama majumba yao kutokana na aibu ya ibara hiyo kwa ndugu zao waumini ambao ni Mashia, na wakihofia masunni wasijekoge kupitia kwao.

Hebu jaribuni kuangalia na kuifikiria hali na mazingira magumu kama hayo wakati huo, lakini pamoja na yote hayo na mazingira hayo magumu na maonevu kama hayo, ugumu wa mazingira kama huu wa hali ya juu, Mashia walikuwa wakisindikiza majeneza ya masunni, hadi  hivi leo Iran ikawa ni yenye itikadi ya Ushia, kwani mateso na maonevu yale hayakuwazuia kutekeleza majukumu yao bali waliendelea na juhudi za kuwaongoza waja na likathibiti na kuwa lile walilo litaka.

Na hapana shaka ya kuwa nyinyi nyote mmesikia jina la Allamah Al-majlisiy, kwa hakika alikuwa ni mwanazuoni mkubwa, na baba yake alikuwa ni miongoni mwa maulamaa wakubwa pia, na katika kizazi chake Allamah Al-majlisiy ambae tangu kufariki kwake hadi sasa kumepita miaka 300 walijitokeza wanazuoni na maulamaa wengi na marajiut- taqlidi na waandishi wa vitabu wakubwa na watoa mawaidha kwa watu, illa tunakuta kuwa babu wa juu kabisa wa Allamah alikuwa ni mfuasi wa madhehebu ya sunni, na vijana wa kishia wa Isfahani waliweza kumkinaisha na yeye kuamua kujiunga na madhehebu ya Shia, pamoja na kuwa zama zile zilikuwa na taasubi kubwa kabisa ya kimadhehebu, lakini ukweli ni kuwa vijana wale walikuwa na hima ya hali ya juu na wakaweza kuwafanya mashia vijana wengine wa kisunni. Nanyi ni juu yenu kufanya kama walivyo fanya waumini na wapigana jihadi hao, na ni wajibu juu yenu kwa ajili ya kulifikia na kulithibitisha lengo hilo au malengo hayo, kwanza kabisa mjifunze vema na muwe ni miongoni mwa maulamaa wakubwa ili muweze kufanya mahojiano na majadiliano na kuwakinaisha.

Na sikilizeni kisa hiki ambacho kilitokea kabla ya miaka arobaini iliyo pita. Wakati  huo tulikuwa Karbalaa, jarida moja la wakati huo liliandika ya kuwa mwanazuini mmoja wa kisunni amekuwa Shia, na walipo muuliza kwa nini umebadilisha madhehebu yako? Akasema: Nimebadilisha kwa sababu ya herufi  moja kati ya herufi za jarri iliyotajwa katika Qur’an tukufu! Wakamuuliza ni herufi ipi hiyo? Akawajibu: Hakika mimi nimesoma Qur’ani mara nyingi sana na mara ya mwisho suratul-fatiha ikanifanya nisite na kusimama katika aya ya mwisho ya sura hiyo, na nilipo anza kusoma suratu (Inna fatahnaa laka fathan mubiinaa) hadi nikafika mwisho wa surat (Muhammad rasulullah walladhina maahu…….) na ambayo inamaanisha maswahaba wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake, na kuona ya kuwa sura inawazungumzia maswahaba wa Mtume na imewataja mara kumi kwa swigha ya jam’u (mfumo wa wingi) au kwa dhamiri za wingi ambazo dhamiri hizo zinawakusudia wao, lakini sura hiyo inapozungumzia ya kuwa malipo na jazaa zao walizo ahidiwa kuwa ni pepo na msamaha na malipo makubwa inasema:

(وعد الله الذ ين آمنوا و عملوا الصالحات منهم)  

(Mwenyezi Mungu amewaahidi wale ambao wameamini na wakafanya amali njema miongoni mwao…)

Kwa hivyo basi herufi ya (Mim) inamaana ya (Baadhi), na herufi hii ilinifanya nifikirie na kujiuliza: Kwa nini Maswahaba wote hawaingii peponi kama tulivyo fundishwa?

Nikajisemea moyoni mwangu: Niwajibu niende na kufanya utafiti na udadisi kuhusu suala hili, na jambo hilo likanipa picha ya kuwa inawezekana suala hili likawa ni miongoni mwa mifumo ya Qur’an, lakini mimi nimeiona aya hii na kuikuta ikiwa wazi kabisa kwani herufi hiyo inamaana ya (Baadhi) ya (Maswahaba) na (sio wote) laa sivyo hakika Qur’an imewataja wote katika aya nyingi tofauti na katika aya  hii, kwa hivyo  nadharia ya uadilifu wa Maswahaba ikiwa imetenguka kwangu, na utafiti wangu ukanifikisha katika natija hii ya kuwa hawa (Baadhi) ya walio tajwa ni wafuasi wa Ali bin Abi Twalib (a.s) na wale walio shikamana na wilaya (utawala) yake na kutokana na utafiti huo nikawa Shia.

Kwa hivyo basi ni juu yenu kuyaandaa vema mambo yenu, na fanyeni juhudi kubwa na wala msipoteze fursa hii ya umri wenu, na someni vizuri na mtwalii sana (someni sana vitabu mbali mbali) mpaka muwe ni miongoni mwa watu wenye elimu, kwani watu wa batili hawana elimu na kila walicho nacho ni njozi za mashetani.

Imam Swaadiq (a.s) amesema: Ni juu yako kuwa na vijana (wenye umri mdogo) hakika wao ni wepesi sana kuelekea kwenye kila la kheri .[4]

Na Al-ahdaath walo tajwa kwenye hadithi ni kizazi kipya, kwani vijana bado akili zao hazija oshwa, na wao ni wepesi zaidi katika kufanya kheri kuliko wengine. Kwa hivyo fanyeni harakati na nashati ili India na ulimwengu wote wawe ni Mashia watupu………..insha allah.  

 

WAOKOENI WATU KUTOKANA NA UJINGA UPOTOVU NA DHULMA KAMA IMAM HUSEIN (A.S) ALIVYO WAOKOA [5]

 

MANENO YA MHESHIMIWA AYA TULLAHIL-UDHMAA IMAM SAYYID SWADIQ SHIRAZIY (Mungu amzidishie umri) ALIYO YATOA KWA MNASABA WA KUMBUKUMBU ZA ASHURA SIKU ALIYO UWAWA SHAHIDI SAYYID SHUHADAA IMAM HUSEIN (A.S)

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu.

 

Sifa zote njema na himidi ni za  Mola wa viumbe wote na sala na salam ziwe juu ya Mtume wake alie muaminifu Muhammad (s.a.w) na Aali zake watwaharifu na laana iwe juu ya maadui zao wote.

Ama baada, hakika Mwenyezi Mungu alie takasika alitaka kwa kufa shahidi Imam Hussein (a.s) kuweka mazingatio, kilio, ibra na kigezo kizuri, si kwa kizazi kilicho fuatia baada yake pekee, bali hata kwa Mitume na Manabii (a.s) ambao Imam Hussein alikuja baada yao (a.s).

Ama kuhusu mazingatio na kilio, kwa hakika alianza kutekeleza mambo hayo Muumba wa viumbe pale alipo muumba Adam (a.s) kwani Jibrilu alimtajia (a.s) watwaharifu watano ambao ni Muhammad, Ali, Fatima, Hassan, Hussein (a.s) na Adam akamwambia: Nina nini mimi kila ninapo mkumbuka Hussein macho yangu hutokwa na machozi, kisha kuamsha huzuni na majonzi yangu, na Mwenyezi Mungu mtukufu akamuambatanisha pamoja na manabii katika visa vyao kupita kwao katika ardhi tukufu ya Karbalaa na matatizo waliyo kumbana nayo katika ardhi hiyo, na hali hiyo ikaendelea katika muda wote mpaka Imam Hussein aliposema (a.s)

أنا قتيل العبرة لا يذ كرني مؤمن إلا بكي

(Mimi ni muuliwa mwenye Ibra (mazingatio) hanikumbuki muumini yeyote isipokuwa hulia).

Ama kuwa kwake ni mazingatio na kigezo, kwa hakika Imam Swadiq (a.s) aliashiria katika ziyara yake aliyo msomea babu yake Hussein (a.s) siku ya kumbukumbu ya  Arobaini ya Imam Hussein huku akimzungumzia Mwenyezi Mungu mtukufu kwa  kumuashiria Hussein (a.s): Na akajitolea damu yake katika njia yako ili awaokoe waja wako kutoka katika ujinga na utata wa upotovu (njia ya upotovu).

Na waja hapa: Haimaanishi kikundi fulani, au umma fulani, au kizazi fulani.

Na Kuokoa: Ni kuashiria kwenye mambo waliyo tihaniwa nayo watu wale. Na bado mtihani huo upo. Kama kutumbukia katika mabalaa ya aina tofauti na mambo ya kila aina ambayo msingi wake ni ujinga na upotovu.

Na Kubabaika: Ambako kumewakumba watu wengi katika mwendo mzima wa maisha yao na mwisho wao (yaani akhera yao).

Hizi ndio nukta ambazo zinaunda sehemu fulani kati ya malengo ya Imam Hussein (a.s) katika kauli zake na matendo yake katika historia ya Ashura.

Ni uzuri ulioje kwa waumini kila  mahala walipo na kila mmoja wao kusimama na kutekekeza jambo hilo la kheri katika nyanja mbali mbali. Na kufanya awezalo kulifanya kama kufanya maandalizi ya kuwafikishia walimwengu wote habari zihusianazo na upande wa kufanya mazingatio na kulia kwa ajili ya Imam, kwa kufanya majlisi ya kumbukumbu za kufa shahidi kwa Imam Husein  na kudhihirisha alama na shiari za Imam Hussein ambazo ndio kitu cha kuendeleza na kudhihirisha alama na shiari za Mwenyezi Mungu alie takasika, na kwa hakika Qur’an tukufu amelisifia jambo hili kuwa ni katika uchaji wa Mwenyezi Mungu

 (من تقوي القلوب).

Na haya ndio ambayo yaliifanya hali ya kulia kwa mfazaiko kusiko kwa kisheria na kuliko kemewa kisheria katika misiba yote, liwe ni jambo lenye kusifika na kuamrishwa kulifanya na kupewa malipo juu ya jambo hilo ikiwa litafanyika kwa ajili ya Ashura, na katika njia ya bwana wa mashahidi Imam Husein (a.s).

Na haya ndio mazingatio na kilio vitu viwili ambavyo vimekuwa mutawaatir na mashuhuri na kupokelewa kwa wingi kutoka kwa Watu wa nyumba ya utume na ujumbe wa Allah (a.s) hadi macho yao yakapatwa na vidonda, na kuhusiana na hilo Imam Ridhaa (a.s) amesema katika hadithi iliyo pokelewa kutoka kwake na Rayyaan bin Shabiib ya kuwa:

 (إن يوم الحسين أقرح جفوننا  )

 (Hakika siku ya Husein Imeyatia vidonda  macho yetu).[6]

Na haya ndio yaliyo sababisha kutokwa machozi macho yale matwaharifu ya walii mtukufu wa Mwenyezi Mungu Imam Mahdi mwenye kusubiriwa (rehma za Mwenyezi Mungu zowe juu yake na Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake na faraja yake tukufu) kama ilivyo pokelewa katika ziara ya (An-nahiyatul-muqaddasa):

(ولأبكين عليك بد ل الد موع  د ما )

(Na kwa hakika nitakulili  damu badala ya machozi).

Na kuhusu mazingatio na kigezo, mambo ambayo Imam Husein (a.s) aliyatangaza na kuyadhihirisha  mara kadhaa wa  kadhaa tangu alipotoka  katika mjiwa wa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu  na kuyarudia katika mji mtukufu wa Makka, na katika muda wote alipokuwa njiani akielekea Karbalaa tukufu, na katika Karbalaa, na katika Usiku wa Ashura, na siku ya Ashura, katika hotuba yake barua zake na maneno yake mbali mbali, na kupitia muamala wake katika mwendo huu wa ushindi, na mazingatio yale ni kusimama kidete kwa kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya kuwatenga pia kuwaepusha watu wote na ujinga na upotovu.

Na haliwezi kuthibitika hilo isipokuwa kwa kufanya  juhudi kubwa na kuwa na ikhlaas kwa ajili ya Mwenyezi Mungu alie takasika. Na kujitolea muhanga kwa kiwango kikubwa na cha hali ya juu katika njia ya kuwaelimisha watu na waja wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na kuieneza nuru ya Ahlul bayti (a.s) kila upande na kila mahala na katika kila mji na kijiji, na katika kila nyumba na  vibanda vya makuti, na kuifikisha kwa kila mtu wanamume kwa wanamke, mabinti kwa vijana.

Na kutekeleza mfumo na mwenendo wa Imam Husein (a.s) katika kuitumia Ashura kwa ajili ya kuwaokoa waja wa Mwenyezi Mungu mtukufu kutokana na dhuluma na mauaji yaliyopo katika zama hizi, umwagaji wa damu, na kuonekana kuwa ni kikundi kidogo chenye kufuata batili na kuadhibiwa, na kudharauliwa kwa mambo matukufu ambayo watu wengi katika siku hizi wamekuwa wakiyavunjia heshima yake, na hasa hasa waislaam katika sehemu tofauti za Ardhi hii.

Na kwa ajili ya kueneza misingi ya Uislaam na matawi yake. Kupitia vyombo vyote vya habari na tabligh. Katika nyanja mbali mbali za maisha.

Na Mwenyezi Mungu ndie mwenye kuombwa msaada awawafikishe wote kupata mazingatio haya na kigezo hiki, na awawafikishe kupata mazingatio pia kutokwa na machozi, nae ndie mwenye kutegemewa.


[1] Moja kati ya hotuba zake aliyo itoa mheshimiwa Swadiq kwa wanafunzi wa Hawzah ya kielimu watokao katika nchi ya India, na alisisitiza katika hutuba hiyo juu ya majukumu wayabebayo  katika kuutumikia Uislaam na kueneza itikadi ya Ahlul baiti (a.s) mwaka 1423.

[2]- suratun-nahli aya 96.

[3]- Al-kafiy juzu ya 5 \ mlango wa Ad-dua ilal-islaam kablal-qitaal, ukurasa wa 36 \ hadithi namba 10.

[4]- Ar-rawdhatu minal-kafiy juzu ya 8 \ hadithi ya Rayyaah \ 93 hadithi ya 66.

[5]- Muharramul-haram mwaka 1423 hijiria.

[6] -Buharul-anwaar juzu ya 44\ mlango wa 34\ hadithi ya 17\ ukurasa wa 283.